HII HAPA HABARI MPYA KUHUSU KAMUSOKO NA DONALD NGOMA - WAPENDA MPIRA

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Saturday, 31 March 2018

demo-image

HII HAPA HABARI MPYA KUHUSU KAMUSOKO NA DONALD NGOMA

Responsive Ads Here
ngoma-kamusoko



Baada ya kuwasilini mjini Singida salama jana, kikosi cha Yanga kinafanya mazoezi ya mwisho leo kwenye Uwanja wa Namfua.


Yanga iliwasili mjini humo ikiwa ina kibarua cha mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Singida United utakaopigwa siku ya Pasaka Aprili Mosi 2018.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, jana alisema wachezaji wote wapo fiti kuanza na jukumu litabakia kwa Kocha George Lwandamina kuamua yupi amtumie.

Taarifa za awali zilidai Kuwa ngoma na kamusoko walikuwa na majeruhi kidogo lakini Taarifa nzuri ni Kuwa wote wako fiti. 

Mchezo huo unataraji kuanza majira ya saa 10 kamili jioni ambapo mshindi ataungana na timu zitakazokuwa zimetinga hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.

Stand United ndiyo timu ya kwanza kuingia hatua ya nusu fainali kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Njombe Mji jana, mechi iliyopigwa Kambarage Stadium.


Post Bottom Ad

Kurasa

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *