- WAPENDA MPIRA

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Thursday, 5 April 2018

demo-image
Responsive Ads Here
InShot_20180331_041608520

  • Timu ya Simba itawakosa wachezaji watatu muhimu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.
Taarifa hizo zimekuja muda mfupi baada ya timu hiyo kumaliza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Njombe Mji juzi kwenye Uwanja wa Sabasaba.
Wachezaji ambao watalazimika kushuhudia mchezo huo wakiwa jukwaani ni Erasto Nyoni, James Kotei na Juuko Murshid ambao wana kadi tatu za njano kila mmoja.
Akizungumza mjini  hapa, kocha msaidizi wa Simba Masoud Djuma, alisema kukosekana kwa wachezaji hao ni pigo, lakini watapambana kupata ushindi.
Nyoni, Kotei na Murshid ni wachezaji wa kikosi cha kwanza na kukosekana kwao ni pigo kwa Simba katika mchezo huo.
Djuma alidai kuwa Simba ina idadi kubwa ya wachezaji, hivyo nafasi zao zitajazwa na wengine aliodai ana uhakika watacheza kwa kiwango bora.
“Kweli inaweza kuwa shida, lakini tutajipanga kuangalia wachezaji gani watacheza katika nafasi zao, kubwa tunataka pointi tatu ni mchezo muhimu kuliko kitu chochote,” alisema Djuma.
Pia Simba inaweza kumkosa beki wa kati Salim Mbonde aliyeumia goti katika mchezo huo wa juzi usiku ambao Simba ilishinda mabao 2-0 yaliyofungwa na John Bocco.
“Itabidi nipate siku mbili za kapumzika nione kama naweza kurudi uwanjani kufanya mazoezi au nipumzike zaidi, lakini kweli nilijitonesha goti, “ alisema Mbonde.
Simba jana ilikwenda kuweka kambi Iringa na Ijumaa inatarajiwa kwenda Morogoro kuikabili Mtibwa Sugar Jumapili wiki hii kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Post Bottom Ad

Kurasa

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *